Thursday, 13 April 2017

Epuka magonjwa ya mara kwa mara kwa kuanza kula vyakula hivi 5



Uimara wa kinga za mwili kwa binadamu ni muhimu sana katika maisha kwani husaidia kumfanya mwanadamu kutozongwa na magonjwa ya hapa na pale na hivyo kuisihi akiwa na afya njema.

Kimsingi kinga za mwili huweza kupanda au kushuka kutokana na aina ya vyakula mhusika anavyokula au vinywaji unavyokunywa, lakini pia hata mtindo mzima wa maisha ya mhusika.

Kimsingi miili yetu iliubwa na Mungu ikiwa na uwezo wa kujitibu wenyewe bila kuhitaji dawa yoyote isipokuwa mwili unaweza kupambana na matatizo kutokana na vyakula unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatufahamu tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

Vifuatavyo ni miongoni mwa vyakula ambavyo  huweza kusaidia kuongeza kinga za miili yetu

1. Matunda
Katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya yule anayekula  matunda.

2. AsaliHapa naamanisha asali iliyo asili kabisa na siyo iliyochakachuliwa hii huweza kusaidia kuimarisha kinga za mwili, unachopaswa kufanya ni kulamba kijiko kimoja cha chakula kila siku kutwa mara tatu kwa mwezi mmoja itasaidia kuimarisha kinga zako za mwili.

3. Ubuyu
Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku kwani juisi hiyo huwa na wingi wa vitami C nyingi ambazo husaidia kuimarisha kinga za mwili.

4. Nazi
Matumizi ya nazi pia huweza kusaidia kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na mafuta yaitwayo ‘medium chain fatty acids’ ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali.

5. Tangawizi

Ni moja ya kiungo ambacho kinaingia kwenye orodha hii ya kuimarisha kinga za mwili pia husaida kumuweka mbali mhusika dhidi ya magonjwa ya viungo yaani mifupa na kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa pia

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku



No comments:

Post a Comment