Tuesday, 11 April 2017

Faida 3 za kutumia maji yenye mchanganyiko wa chumvi


Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com karibu tena tuendelee kufahamishana  mambo kadhaa kuhusu mimea, matunda na mbinu mbalimbali za kiasili za kuboresha afya zetu.

Leo naomba nikwambie kuhusu faida za matumizi ya maji yenye mchanganyiko wa chumvi:-

1. Kwanza husaidia kumaliza tatizo la harufu ya miguu
Unachopaswa kufanya ni kuandaa maji ya uvuguvugu kisha weka kwenye beseni na kuchanganya na chumvi halafu weka miguu yako kwenye beseni lenye maji hayo kwa dakikia kadhaa zisizopungua tano. Fanya hivyo kila siku angalau kwa wiki mbili mfululizo.


2. Husaidia kukuza kucha 
Kuna baadhi ya watu kucha zao huchukua muda kidogo kukua hasa kucha za miguuni, sasa unachoweza kufanya ni kuandaa maji yenye mchanganyiko wa chumvi kisha utaloweka miguu yako kwenye maji hayo kwa dakika 15

3. Husaidia kushusha joto la mwili (fever)
Unachopaswa kufanya ni kupata kikombe kimoja chenye mchanganyiko wa kijiko kidogo cha chumvi kisha andaa kitambaa kisafi na kukichovya kwenye maji yenye mchanganyiko wa chumvi na baadaye utamkanda mhusika sehemu zenye joto kali la mwili.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment