Wednesday, 19 April 2017

Faida 4 za kiafya utakazozipata kwa kucheka tu!


Wataalam wa saikolojia wanasema kuwa kucheka au kufurahi ni moja ya tiba kwa afya ambayo huifanya miili yetu kubaki na afya bora zaidi.

Naomba leo nikwambie haya mambo kadhaa ambayo utayapata endapo utakuwa ni mtu wa kucheka na kufurahi.

1. Kwanza kabisa kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongo wa mawazo na kumfanya mhusika kuwa vizuri kiakili.

2. Husaidia kuimarisha afya ya mapafu
Unapocheka husaidia mapafu yako kutanuka na kuingiza ndani hewa ya safi yaani oxygen. Hivyo unapocheka zaidi tambua kuwa unasaidia kiwango cha hewa kuingia cha kutosha ndani ya mwili na kusaidia damu kusambaa vyema mwilini.

3. Husaidia kuboresha utendaji kazi wa moyo
Kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kukuweka mbali dhidi ya shinikizo la damu la kushuka, kwa sababu husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini na pia kusaidia mishipa ya damu kutenda kazi vizuri.

4.Huboresha kinga za mwili
Kucheka ni muhimu kwani husaidia kuongeza homoni za hisia ndani ya mwili. Kutokana na mabadiliko hayo huenda kusaidia kuimarisha kinga za mwili.

Kwa maelezo zaidi au ushauri wasilina na Mtaalam Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment