Thursday, 13 April 2017

Faida 7 muhimu zitakazoingia mwilini mwako kutokana na kutumia ubuyu


Mwenyezi Mungu ametujalia kuwa na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake ya kuwepo hapa juu ya ardhi.

Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu. 

Zifuatazo ni faida 7 za ubuyu kiafya
1. Ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana kwenye machungwa.

2. Ubuyu pia umesheheni kiwango kikubwa cha madini ya calcium zaidi ya kile kinachopatikana kwenye maziwa ya ng’ombe.

3. Pia ndani ya ubuyu kuna madini ya chuma, magnesiamu pamoja na potasiamu. madini ya magnesium husaidia kujenga afya ya mifupa.

4. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini

5. Ina virutubisho vyenye uwezo wa kulinda mwili kutokana na kuwa na vitamin C yakutosha

6. Huongeza nuru ya macho

7. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment