Friday, 21 April 2017

Fanya mambo haya matano ili uongeze uwezo wako wa kufikiri mara dufu

Uwezo wa kufikiri kati ya mtu mmoja na mwingine unaweza kutofautiana kutokana na sababu mbalimbali za kiumbaji kama ilivyo kwa uwezo wa kufikiri kati ya mwanaume na mwanamke.

Inaelezwa kuwa mwanamke anauwezo wa kufikiri mambo mengi kwa wakati mmoja na kwa haraka, lakini mwanaume hawezi kufikiri mambo mengi kwa wakati mmoja na huwa anafikiri kwa taratibu mno kuliko mwanamke.

Kutokana na mwanaume kufikiri taratibu humsaidia pia mambo yake kufanya kwa umakini au kuzungumza kitu baada ya kukifikiria sana akilini mwake, lakini mwanamke kutokana na kufikiri kwake kwa haraka haraka kuna wakati huchangia kufanya maamuzi ambayo hata wao baadaye hujikuta wakiyajuitia na ndio maana si ajabu kusikia mwanamke akisema mimi sikujua kama ingekuwa hivi au vile .

Hata hivyo, hiyo si mada yangu leo hapa kikubwa nimelenga kutaka kukueleza kuhusu namna unavyoweza kuongeza uwezo wako wa kufikiri zaidi.

1. Fanya mazoezi
Mazoezi husaidia kuchangamsha chembe hai za ubongo kwa kupitia mfumo wa neva, lakini pia mazoezi haya haya husaidia kupunguza msongo wa mawazo.

2. Penda kujisomea
Kusoma pia husaidia kuongeza uwezo wako wa kufikiri, unaposoma vitabu mbalimbali mfano vya kuhusu biashara, afya, saikolojia n.k itakusaidia kufikiria zaidi kuhusu yale utakayoyasoma.

3. Zingatia mpangilio wa mlo wako
Vyakula mfano wa kitoweo cha samaki unapokula angalau mara tatu kwa wiki huweza kukusaidia kuongeza uwezo wako wa kufikiri, lakini pia hata juisi ya nanasi nayo inanafasi ya kuongeza uwezo wa kufikiri kwako.

4. Usiogope kuendelea kujifunza
Hakikisha  kila siku au kwa wiki basi unajifunza mambo kadhaa ambayo awali ulikuwa huyafahamu, lakini hakikisha mambo hayo yana tija katika maisha yako ya kila siku.

5.  Fanya Mazoezi ya Ubongo
Mazoezi haya ya ubongo ni pamoja na kucheza michezo inayoshughulisha akili yako kama "Draft" n.k.

Zingatia
Kama ukiyafanya hayo naamini pia itakuwa rahisi hata kwako kuweza kufanikiwa katika biashara zako au kazi zako kwasababu utafikiria vizuri namna ya kuongeza thamani kwenye biashara yako au kazi zako.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment