Saturday, 22 April 2017

Hivi ndivyo nguvu zako za kiume zinavyoweza kuathiriwa na mzunguko wa damu hafifuKama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii naamini utakuwa umeshafahamu umuhimu wa mzunguko mzuri wa damu ndani ya mwili.

Sasa saizi naomba nikueleza kuhusu ishara au dalili zinazoonesha kuwa mzunguko wa damu mwilini haupo sawa yaani ni hafifu.

1. Kuhisi baridi mikononi na miguuni
Mzunguko wa damu unapokuwa hafifu huchangia joto la mwili kushuka pia na hivyo kusababisha hali ya ubaridi hususani kwenye mikono na miguuni.

2. Mwili kuhisi uchovu
Mwili unapokosa mzunguko mzuri wa damu kimsingi hata hewa ya oxygen huwa si ya kutosha sana na hivyo huchangia mhusika kuhisi hali ya uchovu na hata maumivu ya viungo pia.

3. Kushindwa kuhimili tendo la ndoa
Hii ni kwa wanaume sana sana kwasababu mzunguko wa damu unapokuwa haupo vizuri inamaana hata damu pia haitakwenda ya kutosha katika via vya uzazi vya kiume na hivyo kuchangia mwanaume kushindwa kufanya ipasavyo tendo hilo.

4. Tatizo la umeng'enyaji wa chakula
Kutokana na mwili kukosa nguvu na kutopata virutubisho vizuri, hivyo hufanya hata viungo vinavyofanya kazi ya umeng'enyaji chakula kutofanya kwa ufanisi unaofaa.

5. Kupungua kwa uwezo wa kufikiri
Unapoona unakuwa mtu wa kusahau mambo kila mara jitahidi ufanye uchunguzi huenda ukawa unashida kwenye mzunguko wa damu kutokuwa vizuri.

6. Kinga za mwili kutokuwa imara
Unapokuwa na mzunguko wa damu usiomzuri huweza kuchangia hata kinga za mwili kutofanya kazi zake vyema kwasababu oxygen haisambai vizuri mwili na hivyo kufikisha virutubisho mwilini kila sehemu kushindikana.

Dalili nyingine  ni pamoja na kukosa hamu ya kula. Kwa leo naomba niishie hapo, lakini unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmanditz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi kutoka kwa Mtaalam Mandai.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment