Friday, 21 April 2017

Hizi hapa njia rahisi za kupunguza uzito

Kuna watu wanapata shida sana kutokana na kuwa na uzito mkubwa, jambo ambalo huwakosesha raha pia.

Leo napenda kukufahamisha hizi mbinu za kukabiliana na kuwa na uzito kupita kiasi hebu jaribu kufuata haya yafuatayo:

Tembea kwa nusu saa asubuhi kisha baada ya kukamilisha mazoezi yako tafuta maji ya uvuguvugu kunywa glasi mbili hadi nne

Jitahidi kunywa supu ya mboga mboga (vegetable soup) pamoja na matunda, huku ukiepuka kula vyakula vyenye mafuta mengi pamoja na kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi pia.

Kuhusu kufanya mazoezi unashauriwa kufanya kabla ya kunywa chai asubuhi. Mazoezi kwa ujumla yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yataambatana na lishe bora.

Kwani kitendo cha kufanya mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, saratani na shinikizo la damu, ni vyema ikafahamika pia kuwa familia ambazo hufanya mazoezi huwa na afya bora.

Mazoezi pia husaidia sana kuboresha tendo la ndoa na hivyo kuleta amani na mahusiano mazuri ndani ya familia kwani mtu anayefanya mazoezi bila kujalisha ni mazoezi ya aina gani basi kwa kawaida huwa na uimara katika afya.

Hayo ni machache tu kuhusu mada hii ya kupunguza uzito endelea kuwa karibu na tovuti hii ili kuyapata mengine zaidi, lakini kama utahitaji ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 784 300 300, +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment