Thursday, 20 April 2017

Hizi ndio faida za kula matunda kwa familia yako


Zipo faida kadhaa za ulaji wa matunda, ukiachilia mbali ladha yake, kwani matunda huwa na vitamin na virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu ndani ya mwiki.

Zifuatazo ni miongoni mwa faida za matunda kiafya.

Ulaji wa matunda husaidia kupunguza hatari ya magonjwa kama vile kiharusi, matatizo  ya moyo, shinikizo la damu pamoja na aina mbalimbali za saratani.

Mfano unapokula embe husaidia kuimarisha uwezo wako wa kuona vizuri kutokana na tunda hilo kuwa na vitamini A na E.

Pia matunda husaidia kuboresha kinga za  mwili mathalani unapokula chungwa mara kwa mara huenda kusaidia kujenga kinga imara za mwili kutokan na tunda hilo kuwa na wingi wa vitamin C.

Matunda mengi yanakiwango kizuri cha nyuzinyuzi ambacho huenda kuboresha afya ya umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Zipo faida nyingi nyingine za matunda lakini kwa sasa naomba tuishie hapo kisha baadaye tunaweza kuelezana mengine zaidi.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/0784 300 300/ 0769 400 800 au barua dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment