Monday, 10 April 2017

Ifahamu juisi hii yenye uwezo wa kukupatia faida 4 kwa mara moja


Zipo juisi za matunda mbalimbali ambazo huwa na faida kadha wa kadha ndani ya miili yetua  ikiwa ni pamoja na kulinda afya zetu kwa ujumla.

Hata hivyo, leo naomba kukwambia haya mamboa manne ambayo utaweza kuyapata ikiwa utaanza kutumia juisi ya tunda la stafeli.

Zifuatazo ni faida muhimu za juisi ya tunda hilo.

1. Huimarisha kinga za mwili.
Juisi ya stafeli husaidia kuimarisha kinga ya mwili kutokana na kuwa na vitamin C yakutosha


2. Huboresha mmeng'enyo wa chakula
Tunda hili limeshsheni nyuzinyuzi yaani fiber ambazo pia hupatikana ndani ya juisi yake hivyo matumizi ya juisi hii huweza kuwa suluhisho kwa wale wenye shida ya umeng'enyaji wa chakula.

3. Huimarisha afya ya mifupa na meno.
Juisi yake ni nzuri kwa afya ya mifupa na meno kwa kuwa imesheheni madini ya phosphorus pamoja na calcium ambayo yote kwa pamoja husaidia kuimarisha afya ya meno na mifupa mwilini.

4. Huondoa uwezekano wa kupungukiwa na damu.

Juisi ya stafeli ni nzuri kwa wale wenye anemia kwani inamadini ya chuma ambayo husaidia kutengeneza seli nyekundu za damu.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment