Saturday, 22 April 2017

Je, kucha zako zinaharibika na kuwa za njano? njia hii asili itamaliza shida hiyo


Moja urembo hasa kwa kinadada ni pamoja na kuwa na kucha nzuri, sasa tatizo huweza kujitokeza endapo kucha zitakosa muonekano mzuri.

Mfano kuna baadhi ya kinadada wamejikuta kucha zao zikiharibika na wasijue nini cha kufanya.

Moja ya kuharibika kwa kucha ni pamoja na kubadilika kwa rangi na kuwa na rangi ya njano ambayo kimsingi hupoteza kabisa muonekano wa kucha na hata mvuto wake.

Sasa basi kama wewe kucha zako zinatatizo hilo la kuwa za njano usijali leo ninaomba nikufunze mbinu hii asili ya kumaliza tatizo hilo.

Unachopaswa kufanya ni kupata limao moja kubwa kisha kamua maji yake kwenye bakuli halafu utatumbukiza kidole chenye kucha zilizobadilika rangi na kuwa za njano yaani Yellow nail kisha usitoe hadi pale zitakapopita dakika 10 hadi 15.

Namna utakavyotakiwa kuloweka kucha zako kwenye maji ya limao kwa dakika 10 hadi 15
Fanya zoezi hilo kila siku asubuhi na jioni kwa wiki kadhaa hadi pale utakapoona mabadiliko na baadaye kucha zako kuanza kung'ara.

Kama hujaelewa vizuri au unahitaji ushauri zaidi kuhusu tatizo hili na hata mengine yanayokusumbua wewe, rafiki yako au ndugu yako usisite kutupigia kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment