Saturday, 22 April 2017

Jifunze namna ya kutumia nyanya ktk kumaliza tatizo la mafuta usoni


Leo Jumamosi naomba tuendelee kufahamishana mambo mbalimbali kuhusu afya zetu na kwa sasa naomba nikufahamishi hizi mbinu za kukusaidia kama ngozi yako (uso) wako unamafuta mengi.

Ni ukweli kwamba unapokuwa na ngozi yenye mafuta mengi hukera kwani muda wote unaonekana kung'aa zaidi hata kama umepaka baadhi ya vipodozi vya kuzuia uso kuwa na mafuta mengi.

Zifuatazo ni njia mbili zitakazokusaidia kumaliza shida hiyo.

1. Tumia Nyanya
Unachopaswa kufanya ni kupata nyanya kisha ioshe vizuri halafu ikate vipande viwili katikati kisha tumia kila kipande kusugua taratibu kuanzia shingoni hadi usoni, lakini hakikisha hautumii nguvu kubwa katika zoezi hili.  Baada ya dakika kadhaa 20 unaweza kunawa uso wako na maji ya uvuguvugu kisha jifute na taulo safi. Fanya zoezi hilo kwa wiki kadhaa hadi pale utakapoona mabadiliko.

2. Juisi ya limao
Andaa juisi ya limao kisha tumia pamba kupaka juisi hiyo ya limao kuanzia shingoni hadi usoni kwa siku kadhaa. Tafadhali hakikisha hautumii nguvu kabisa wakati wakusugua kwani huweza kuharibu ngozi yako usipokuwa makini.

Kama hutahitaji maelezo zaidi kuhusu mada hii naomba wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.
No comments:

Post a Comment