Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 5 April 2017

Jifunze njia hii ya kutunza nywele zako bila kwenda saloon kila wiki? soma hapa

Ni ngumu kuamini kuwa majani ya mpera yanaweza kuwa sehemu ya bidhaa inayoweza kubadili muonekano wako mwanamke na kukufanya kuonekana mrembo zaidi hususani katika upande wa nywele zako.

Hi ni kutokana na majani hayo kuwa na uwezo wa kuzilinda nywele zako kutokatika hovyo na kuzifanya kukua vizuri na kuendelea kuonekana na afya bora.

Nimeona nikuletee hii kwani naamini inaweza kuwasaidia wale wasio na uwezo wa kwenda saloon kila wiki, hivyo wataweza kutumia mbinu hii asili kuendelea kuboresha afya nywele zao.

Jambo la kufanya ni kupata majani hayo ya mpera kiasi cha fungu moja kama la mboga ya majani kisha chemsha kwa muda usiopungua dakika 15 hivi na uyaache yapoe.
Mwanamke akiosha nywele zake kwa maji yatokanayo na mpera

Baada ya hatua hiyo chukua maji ya hayo yachuje kisha ubaki na maji ya mpera tu bila majani yake na uanze kutumia maji hayo kuoshe nywele zako, huku ukihakikisha yanafika hadi kwenye mzizi wa nywele zako.

Baada ya hapo acha kwa dakika kadhaa kisha utaosha nywele zako na baadaye kupaka mafuta yako unayotumia, yanaweza kuwa ya nazi ili kupata matokeo mazuri. Kumbuka kuwa maji ya majani hayo ya mpera pia husaidia kuondoa hata tatizo la mba kwenye nywele.

Fanya zoezi hilo mara kwa mara bila shaka baada ya muda fulani utaanza kujionea mabadiliko ya afya za nywele zako.

Kwa msaada zaidi unaweza pia kutupigia simu kwa namba zifuatazo: 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment