Thursday, 6 April 2017

Kwa wale ambao si watumiaji wa miwa (juisi) basi wanazikosa faida hizi 5 mwilini mwao

Sugarcane Juice in Glass - Sugarcane juice benefits
Kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Tanga na mikoa kadhaa ukizungumzia juisi ya miwa wengi wanaweza kuifahamu vizuri.

Ni moja ya juisi ambayo imepata wanywaji wengi katika kipindi cha hivi karibuni wakiwemo wanaume kwa wanawake, lakini zaidi wanaume.

Hata hivyo, wengi wanaotumia juisi hii sina imani kama wanajua umuhimu wake, lakini asilimia kubwa wanaitumia tu kama moja ya kiburudisho kutokana na kuwa ladha nzuri na tamu mdomoni.

Sasa leo naomba nikueleze baadhi ya faida hizi 5 za unywaji wa juisi hii ya miwa.

1. Husaidia kuimarisha kinga za mwili kwa sababu ya kuwa na utajiri wa kirutubisho kiichwacho antioxidants  

2. Pia juisi hii hutumika kuongeza nguvu mwilini pamoja na kuusaidia mwili kupambana na hali ya uchovu pia.

3. Kutokana na juisi hii kuwa na kiwango cha kutosha cha madini ya potassium hivyo inakuwa na uwezo pia wa kupunguza athari za kukosa choo.

4. Matumizi ya juisi hii pia husaidia kupunguza makali ya vidonda vya tumbo kwa muda lakini inamaana si suluhisho la kudumu.

5. Ndani ya juisi kuna madini ya calcium pamoja na potassium ambayo kwa pamoja husaidia kuimarisha afya na uimara wa mifupa.

Moja kati ya madhara ambayo huweza kujitokeza kwa kunywa juisi hii mara kwa mara ni pamoja na kuongeza uzito wa mwili kwa haraka.

Kumbuka kuwa pia tunaweza kukushauri kuhusu matumizi ya lishe bora  na vitu vya asili tupigie sasa kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment