Thursday, 27 April 2017

Limao humaliza tatizo la miguu kuwaka moto

Miguu na nyayo kuwaka moto ni aina ya matatizo ambayo huwapata zaidi watu ambao shughuli zao zinawalazimisha kutembea kwa mda mrefu au kusimama kwa mda mrefu pamoja na kukaa kwa mda mrefu miguu ikiwa imening'inia.

Hata hivyo, tatizo hili huchangiwa na mzunguko dhaifu wa damu katika miguu na ukosefu wa virutubisho na madini yanayohitaji ndani ya mwili.

Moja ya mbinu ya kumaliza tatizo hili ni pamoja na kutumia zaidi chakula cha asili ambacho husaidia kupunguza sumu ndani ya mwili pamoja na kufanya mabadiliko katika aina ya vyakula vitakavyoliwa kwa ajili ya kupata virutubisho na madini.

Ifuatayo ni moja ya mbinu ambayo huweza kutumika kukabilia na tatizo hili:-

Unachopaswa kufanya ni kuosha miguu yako kwa maji ya moto na sabuni kisha kata limao katika vipande viwili, halafu tumia kwa kupaka sehemu unazojisikia kuungua au kuwaka moto kwenye miguu yako. Fanya zoezi hilo kwa wiki tatu mfululizo asubuhi na jioni.

Hiyo ni mojawapo kati ya mbinu ya kumaliza tatizo hili ikiwa utahitaji kuzifahamu njia nyingine unaweza kutupigia simu sasahivi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment