Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 6 April 2017

Makosa manne ambayo wabongo tunayafanya kila wakati wa kula


Watu wengi huwa tunamaswali mengi kuhusu ni vitu gani tule na vipi tusile na kwa wakati gani pia ambao utakuwa sahihi zaidi kula vitu hivyo?

Lakini si kila mtu anaweza kuyajibu maswali hayo kwa ufasaha zaidi naomba hapa leo nikueleze mambo yakuzingatia mara baada ya kumaliza kula kila siku.

1. Epuka kunywa maji mara tu baada ya kumaliza kula
Kufanya hivyo kutachangia kuharibu mfumo mzima wa mmeng'enyo wa chakula na hivyo kufanya chakula kushindwa kufanya kazi zinazohitajika vyema ndani ya mwili. Badala yake unaweza kunywa maji hayo mara baada ya dakika 45 au saa moja tangu unapomaliza kula.

2. Epuka kula matunda mara tu baada ya kumaliza kula
Haishauriwi ulaji wa matunda mara unapomaliza kula chakula kwasababu chakula na matunda kwa mda mmoja huvuruga pia mpangilio mzima wa umeng'enyaji chakula ndani ya mwili.

Ulaji wa matunda unaweza kuleta matokeo mazuri unapokula saa moja kabla ya mlo au saa moja hadi mbili baada ya mlo wako.

3. Usilale mda mfupi baada ya kula.
Hii nayo huchangia kuharibu utaratibu mzima wa umeng'enyaji chakula tumboni na kufanya mwili kutopata mahitaji ya kwenye chakula inavyopaswa.  Hivyo unashauriwa kulala mara baada ya saa moja hadi mawili tangu unapomaliza kula.

4. Epuka kutembea muda mchache mara baada ya kula
Unapotembea mara tu baada ya kula tambua unachangia mwili kushindwa kunyonya vizuri virutubisho muhimu vilivyomo ndani ya chakula kutokana na kuvuruga pia umeng'enyaji wa chakula tumboni. Katika hili inashauriwa ipite angalau nusu saa hadi saa moja na nusu ndio uanze kutembea baada ya kula hii najua inaweza kuwa mtihani kwa ndugu zangu tunaokula kwa mamantilie lakini ukweli ndio huo.

Kumbuka kuwa pia tunaweza kukushauri kuhusu matumizi ya lishe bora na vitu vya asili tupigie sasa kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment