Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 1 April 2017

Mambo 4 ambayo mwanamke huyafanya anapotaka kuvunja uhusiano


Picha kwa msaada wa mtandao
Leo ni weekend naomba zaidi tuzungumze kuhusu mapenzi ili kuweza kuboresha mahusiano kuanzia yale ya wachumba pamoja na wanandoa kwa ujumla. Karibu

Katika kuanza mada hizi za mapenzi leo naomba tuzifahamu hizi dalili ambazo huashiria mwanamke uliyenaye yupo katika harakati za kutaka kuvunja uhusiano wenu na hii naamini itawahusu zaidi wanaume.

Kwanza kabisa kwa kawaida huwa kuna ugumu kidogo wa kufanya maamuzi kati ya mwanaume na mwanamke, lakini pindi utakapoona dalili hizi zifuatazo basi tambua kuwa mwanamke uliyenaye yupo katika mikakati ya kufanya maamuzi ya kuachana nawe katika mahusiano.


1. Kujitenga
Mwanamke ambaye anaelekea kufanya maamuzi ya kuvunja mahusiano mara nyingi huanza kuonesha kujitenga. Anaweza kuanza kujitenga kuanzia kwenye kula, kukaa nk.


2. Kukosoa kila kitu
Mwanamke ukiona kila unachofanya au unaongea yeye anakosoa tu basi tambua huyo yupo  katika harakati za kutaka kuvunja uhusiano wenu. Inawezekana mwanamke huyo mwanzoni alikuwa mnyenyekevu na msikilizaji mzuri na mkosoaji kwenye vitu vya msingi tu na tena anakosa kwa nidhamu, lakini anapochoka kwenye mahusiano utaona kila jambo yeye anakosoa tu liwa baya au zuri.

3. Kuondoa utegemezi
Mwanamke ambaye anatamani kuvunja uhusiano huanza kuacha utegemezi kwa mwanaume wake, ikiwa alikuwa anakuomba fedha za matumizi , nauli, ada na matumizi mengine na sasa hakuombi, lakini mambo yake yanaendelea kwenda tu bila myumbo wowote basi tambua kuwa tayari mnaelekea kuachana na mwanamke wa aina hiyo.

4. Kuanzisha mahusiano mapya
Mara nyingi hii huwa hatua ya mwisho ya kukamirisha lengo lake hilo la kuachana na akifika katika hatua hii sasa inamaana anakuonesha yale yote aliyokuwa amedhamiria tangu awali. Hivyo ukiona imefikia hatua hiyo tambua kuwa huna chako tena hapo na uangalie utaratibu mwingine tu.

Kwa mengine mengi kama haya yanayohusu masuala ya mapenzi na mahusiano usiache kusikiliza kipindi cha NJOZI NJEMA kila Jumatano saa nne usiku kupitia TBC FM hapo utakutana na Mtaalam Mandai pamoja na Salome Baptister na kuyajua mengi zaidi kuhusu mahusiano.

Kwa maelezo zaidi au ushauri kuhusu matumizi ya mafuta haya ya mzaituni usisite kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment