Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 7 April 2017

Mambo 6 ya kuzingatia ili kuepuka magonjwa ya moyoMiaka ya hivi  karibuni imekuwa ikielezwa kuwa magonjwa yasiyoambukiza hususani yakiwemo ya  moyo yamekuwa yakishika kasi na kusumbua watu wengi kwa ujumla.

Hata hivyo,  kuna njia ambazo huweza kumsaidia mtu kuepukana na magonjwa ya moyo, hii ikiwa ni pamoja na namna ya mpangilio wa vyakula sambamba na kufanya mazoezi.

1. Unaweza kuepuka magonjwa ya moyo kwa kupendelea kula matunda, mboga za majani pamoja na vyakula vya nafaka ambavyo husaidia kuondoa hatari ya kupata magonjwa ya moyo.


2. Kuepuka matumizi ya sigara na tumbaku, ambayo yote huweza kuchangia mhusika kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Hivyo endapo umekuwa ni mtumiaji wa sigara au tumbaku ni vyema ukafanya maamuzi ya kuacha mara moja ili kujiondoa katika hatari ya kupata magonjwa haya ya moyo.


3. Epuka kuwa na uzito kupita kiasi, hali hii huweza kuchangia mwili kulundikana na mfuta hatari yaani 'cholesterol', ambayo huwa ni hatari kwa afya ya moyo, hivyo ni vizuri ukajenga mazoea ya kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara ili kuepuka kuwa na uzito uliokithiri.


4. Punguza matumizi ya chumvi kupita kiasi, ulaji wa chumvi kupita kiasi kwani huchangia msukumo wa damu kuwa juu zaidi ambayo ni moja ya sababu inayoweza kuchangia mhusika kuanza kukumbwa na tatizo la shinikizo la damu. Pia epuka vyakula ambavyo vimesindikwa kwa chumvi nyingi.


5. Jitahidi kulala kwa muda wa kutosha angalau masaa 7 hadi 8 kwa siku, kukosa usingizi huweza kusababisha mtu kukosa furaha na kuwa mchangamfu na hata shambulio la moyo, kulala usingizi mzuri hutengeneza mtu kuwa mchangamfu na uwezo mzuri wa kupambanua mambo.


6. Jambo la muhimu pia ni kuepuka msongo wa mawazo au kukabiliana na msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo (stress) huweza kusababisha shambulio la moyo (heart attack) na mara nyingine hata kifo. Kufanya mazoezi ni moja ya njia inayoweza kukusaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Zingatia
Pamoja na hayo yote, lakini kumbuka kwamba ni muhimu sana kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya yako mara kawa mara.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment