Tuesday, 18 April 2017

Mambo manne yanayoweza kusababishwa na kukithiri kwa msongo wa mawazo


Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na msongo wa mawazo kutokana na sababu za hapa na pale ikiwa ni pamoja na changamoto za kimaisha, mahusiano n.k

Hata hivyo, msongo wa mawazo si jambo la kuliendekeza sana kwani huathiri afya zetu kwa kiwango kikubwa pia.

Leo naomba nikwambie hizi athari 4 ambazo huweza kuchangiwa na hali ya msongo wa mawazo hasa pale inapokithiri.

1. Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara
Kama huwa hauumwi na kichwa mara kwa mara, lakini ghafla hali hiyo ikaanza basi tambua kuwa huenda msongo wa mawazo ukawa ni sababu.

2. Uso kupatwa na vichunusi vya hapa na pale
Unapoona uso wako umeanza kutokwa na vichunusi vya hapa na pale huenda pia miongoni mwa sababu ikawa ni msongo wa mawazo pia.

3.Kuna wakati stress pia huweza kuchangia kuharibika kwa nywele ikiwa ni pamoja na kukatika kwa nywele hivyo unapoona nywele zako hazikui vyema wakati unazihudumia vizuri tatizo huweza kuwa ni hilo la msongo wa mawazo pia.

4. Akili kushindwa kufanya kazi vizuri
Kuna wakati unaweza kuwa unafikiria kitu cha kufanya halafu baada ya mda fulani unajikuta umesahau kabisa kile ulichokuwa unawaza na wala hukumbuki kabisa, hiyo huwa si dalili nzuri na mara nyingi huashiria kuwa msongo wa mawazo umezidi kwako hivyo unahaja ya kujikwamua hapo ulipofika kabla madhara hayajawa makubwa zaidi.

Kwa maelezo zaidi au ushauri wasilina na Mtaalam Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment