Saturday, 15 April 2017

Mlonge unavyoweza kukusaidia kiafya


Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii bila shaka umekuwa ukijifunza mambo mengi hasa kuhusu mimea tiba pamoja na lishe mbalimbali hususani zile za asili.

Leo nimeona nikwambie msomaji wangu kuhusu majani ya mlonge ambavyo huweza kuwa na manufaa ya kiafya ikiwa zitatumika vizuri na kuandaliwa inavyopaswa.

Majani ya mlonge yanapotengenezwa kama juisi hutumika kusafisha tumbo na kutuliza magonjwa mbalimbali yakiwemo yale ya zinaa.


Pia juisi hiyo ina uwezo wa kuwasaidia wale wenye presha (BP) na kutoa ahueni kwa wale wenye shida ya kisukari kwa kudhibiti kiwango cha sukari ndani ya mwili

Aidha, majani hayo ya mlonge pia huweza kupakwa mwilini kwa lengo la kutibu majipu na maambukizi ya ngozi ikiwa ni pamoja na matangotango.

Pamoja na hayo, tafiti mbalimbali za kisayansi zimekuwa zikiainisha kuwa majani ya mlonge ni chanzo kizuri cha virutubisho kama vile vitamin C, A, pamoja na madini ya Calcium na Potassium pambayo ni muhimu pia ndani ya mwili.


Uwepo wa madini kama calcium na potassium pia unaelezwa kuwa na faida kwa wanaume kwani ni miongoni mwa madini ambayo huwa na mchango wake katika suala nzima la masuala ya uzazi (tendo la ndoa)

Kuna mengi yakuyafahamu kuhusu majani haya ya mlonge na faida zake na si rahisi kuyaeleza yote hapa, hivyo kama utapenda kujua zaidi na namna nzuri ya kutumia majani haya piga simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.co

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment