Friday, 14 April 2017

Namna 2 za asili za kuondoa vinyama vinavyoota kwenye ngozi yako


Kuna vinyama ambavyo huota kwenye ngozi hasa mikononi karibu na vidole na maeneo mengine pia.

Tatizo hili baadhi ya watu huita visunzura inawezekana na wewe ukawa unalifahamu tatizo hili kwa jina jingine kulingana na asili yako.

Sasa leo naomba nikwambie hizi njia ambazo huweza kusaidia kuondoa tatizo hilo.

1. Kitunguu swaumu
Unachopaswa kufanya ni kusaga kiungo hiki kisha weka kwenye sehemu iliyo na tatizo jioni wakati wa kulala na ufunike kwa bandege hadi asubuhi . Kisha asubuhi osha sehemu hiyo kwa maji ya uvugvugu.

Rudia zoezi hilo kila mara hadi pale tatizo litakapoisha.


2. Alovera
Tumia ute wa alovera ambao ni fresh kabisa na upake kwenye eneo lenye tatizo na usugue kwa taratibu kwa dakika kadhaa wakati wa kupaka. Hakikisha ute wote umeingia kwenye ngozi ndipo uache.

Fanya zoezi hili angalau mara tatu kwa wiki mbili mfululizo


Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment