Saturday, 22 April 2017

Nguvu kuu 5 alizonazo mwanamke, ambazo si rahisi kuzitambuaYapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kuwa magumu kidogo kwa wanaume, lakini kuna baadhi ya mambo pia kwa wanawake huwa ni rahisi kutokana na namna walivyoumbwa.

Sasa leo naomba kukwambia hizi aina 5 za nguvu za asili ambazo hupatikana ndani ya mwanamke.

1. Wanawake wananguvu kubwa ya ushawishi kuliko wanaume na ndio maana makampuni mengi huwatumia kinadada katika kitengo cha masoko.

2. Nguvu ya uwezo wa kujadili kuhusu gharama, wanawake wengi si wepesi wa kutoa pesa hovyo pasipo kujadili bei ni lazima wajadiliane bei sana ndipo wanunue hali hii ipo tofauti sana kwa wanaume.

3. Wanawake wanaushawishi sana kwa watoto, inawezekana ushawishi huo ni wa manufaa au hasara, lakini cha msingi hapa itambulike kuwa mwanamke akiamua jambo lake na akitaka mtoto pia aamini hivyo hawezi kushindwa kamwe.

4.Pamoja na hayo wanawake pia wamejaliwa uwezo wa kuyatambua ya mbele, kwa kifupi wanawake wananguvu zaidi kwenye vinywa vyao kuliko nguvu za miili yao , lakini athari za kutotumia vinywa vyao vizuri huwa ni kubwa zaidi.

5.Pia wanawake huwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja bila kuathiriana kati ya jambo moja na jingine kitu ambacho kwa wanaume si rahisi kuweza kufanya hovyo.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment