Monday, 24 April 2017

Njia 2 za asili zitakazomsaidia mgonjwa wa kisukari

Ugonjwa wa kisukari ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza, ambayo husababishwa baada ya kongosho kushindwa kutengeneza 'insulin' ya kutosha ndani ya mwili.

Insulin ni homoni ambayo kazi yake kubwa ndani ya mwili ni kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wanaeleza kuwa  watu waliokuwa na  kisukari mwaka 1980 walikuwa ni milioni 108 na ilipofika mwaka 2014 idadi hiyo iliongezeka zaidi na kufikia wagonjwa milioni 422 duniani kote. 

Pamoja na hayo, inakadiriwa kuwa mwaka 2012 kuna vifo milioni moja na laki tano ambavyo vilisababishwa moja kwa moja na ugonjwa wa kisukari.

Kutokana na madhara hayo ya ugonjwa huo leo nimeona nikueleze kuhusu njia asili ambazo huweza kupunguza madhara ya ugonjwa wa kisukari.

1. Mdalasini
Pata unga wa mdalasini kisha changanya na maji ya moto kisha kunywa maji hayo kila siku asubuhi na jioni kwa lengo la kuondoa changamoto zote za ugonjwa wa kisukari na kumpatia nafuu mgonjwa.

2. Mbegu za uwatu.
Unachopaswa kufanya ni kuloweka mbegu hizo usiku kucha kwenye maji. Kisha asubuhi kunywa maji hayo. Fanya hivyo kila siku ili kupata nafuu kama unasumbuliwa na kisukari.

Kwa maelezo zaidi kuhusu njia hizi mbili au ufafanuzi wa kina usisite kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Zingatia
Ni vyema kuwasiliana nasi ili kupata utaratibu mzuri wa kutumia njia hizo za asili.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment