Saturday, 22 April 2017

Njia 3 asili za kuboresha mzunguko wa damu mwilini mwako


Kwa kawaida miili yetu huhitaji damu kuzunguka vizuri ili shughuli zote ziweze kwenda sawia ndani ya mwili.

Inapotokea mzunguko wa damu mwilini ukawa hafifu huweza kusababisha madhara kadhaa mfano maumivu ya viungo na kwa wanaume pia huweza kuchangia hata upungufu wa nguvu za kiume.

Sasa leo naomba nikueleze msomaji wangu kuhusu hizi njia tatu ambazo zitakusaidia kuimarisha mzungunguko wa damu mwilini.

1. Kufanya mazoezi
Mazoezi pia yanayo nafasi kubwa ya kuimarisha mzunguko wa damu mwilini inaweza kuwa ni mazoezi ya kutembea, kukimbia au hata kuruka kamba n.k.

2. Uchuaji wa mwili (Body Massage) 
Njia hii nayo huweza kuboresha mzunguko wa damu ndani ya mwili ambapo unaweza kufanya zoezi hilo la kuchua mwili kwa kutumia mafuta ya asili kama vile mafuta ya mzaituni n.k.

3. Kuoga maji ya uvuguvugu
Hapa unashauriwa kuandaa maji yenye kiwango fulani cha joto kisha oga maji hayo, hii pia itasaidia sana kuboresha muznguko wa damu ndani ya mwili wako.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment