Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 15 April 2017

Njia 4 za asili za kumaliza michirizi ya mwili


Michirizi mwilini ni moja ya changamoto ambayo huweza kumkuta mtu yoyote katika maisha, lakini zaidi tatizo hili huwakumba hasa kinamama hususani wale wenye miili mikubwa.

Wanawake wengi wamekuwa wakikwazika na tatizo hili la michirizi mwilini, ambapo hali hiyo hutokea zaidi sehemu zenye nyama nyingi kama vile sehemu ya juu ya mikononi, tumboni na mapajani pia.

Leo naomba nikueleze hizi mbinu nyingine za kumaliza tatizo hilo la michirizi.

1. Mafuta ya mnyonyo
Unatakiwa kupata mafuta hayo kisha tumia kwa kupaka sehemu yenye tatizo halafu sugua taratibu kwenye eneo hilo. Fanya hivyo kwa siku mara mbili kwa kipindi cha mwezi mmoja mfululizo na utaona mabadiliko.

2. Mafuta ya mzaituni
Pia mafuta haya nayo huweza kuondoa tatizo hilo kwa kufanya kama utakavyofanya kwa mafuta ya mnyonyo, lakini pia mafuta haya huweza kupunguza hata tatizo la ikunjo mwilini.

3. Ute wa yai
Yai ambalo linatakiwa kutumika hapa ni yai la kienyeji ambapo utapakaute huo wa yai kwenye michirizi na kusugua taratibu. Yai linauwezo wa kuondoa michirizi hiyo kwasababu ya kuwa na vitamin A ya kutosha pamoja na 'collagen'. Tumia ute huo kwa wiki tatu hadi nne mfululizo.

4. Juisi ya viazi mviringo
Unachopaswa kufanya ni kukata vipande vya viazi kisha utatumia kipande kimoja kimoja kusugua taratibu sehemu yenye michirizi. Fanya zoezi hili kwa wiki 3 hadi 4 mfululizo.

ZINGATIA
Unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi kuhusu virutubisho asili vya aina mbalimbali, tunapatikana Ukonga, Mombasa mtaa wa Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au tupigie simu kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 3000/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila sikuNo comments:

Post a Comment