Saturday, 15 April 2017

Njia 4 za asili za kumaliza tatizo la weusi shingoni na kwapani


Leo Jumamosi tutakuwa tukiongea zaidi kuhusu masuala ya urembo na kwasasa naomba nikwambie kuhusu njia za asili za kuondoa hali ya uweusi ambao hutokea shingoni.

Ukiangalia shingo za watu wengi utaona zinautofauti wa rangi ukifananisha na rangi ya sura zao mara nyingi shingo huwa na weusi kidogo huenda kutokana na wengi kusahau eneo hilo la mwili wakati wa kufanya usafi wa mwili (kuoga).

Hapa ninazo njia 4 zitakazobadilisha rangi ya shingo yako kutoka kwenye uweusi na kuwa katika rangi yako halisi.

1. Ganda la chungwa
Pata maganda ya chungwa kadhaa kisha yaanike kwenye jua yakauke halafu saga na upate unga wake kisha unga huo changanya na maziwa freshi kidogo kulingana na wingi wa unga wa maganda ya chungwa hakikisha isiwe nyepesi sana.

Baada ya hapo utatumia mchanganyiko huo kusugulia shingoni kila unapoanza kuoga ukisha sugua acha dakika kumi kabla ya kuondoa mchanganyiko huo. Fanya hivyo kwa wiki kadhaa na utaona mabadiliko.

2. Tango 
Andaa juisi yako ya tango kisha utachanganya na juisi ya limao halafu utautumia mchanganyiko huo  kwa kusugua kwenye shingo na uuache mchanganyiko huo kwa dakika 10 kabla ya kuondoa mwilini mwako.

3.Juisi ya kiazi mviringo
Andaa viazi vyako kadhaa kisha visage na upate juisi yake iwe nzito kisha tumia juisi mchanganyiko huo kusugu kwenye sehemu ya shingo ambayo inaweusi kutokana na kutofanyiwa usafi mara kwa mara.

4. Alovera
Tumia ute ute wa alovera kusugua taratibu sehemu ya shingo yako kisha acha mchanganyiko huo kwa dakika 20 kabla ya kunawa. Fanya zoezi hilo hadi utakapoona mabadiliko.

Zingatia
Njia zote hizo huweza pia kutumika kumaliza tatizo la weusi kwapani pia

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment