Thursday, 13 April 2017

Njia 5 rahisi za kushusha joto la mwili


Kuna wakati jito huwa linakuwakali kiasi kwamba unajiuliza utumie kitu gani cha kushusha ukali wa joto hilo.

Wengi wanapoona hivyo huwaza kunywa maji ya baridi sana ambayo nayo huweza kuleta madhara ikiwa ni pamoja na 'tonsillitis' .

Baadhi yao huwaza pia kushusha joto hilo kwa kuoga maji ya baridi sana ambayo husaidia kutuliza joto la mwili kwa muda mfupi tu, lakini baada ya kumaliza kuoga joto hurudi palepale.

Sasa leo ninazo mbinu nyingine za kusaidia kushusha joto kali la mwili kama ifuatavyo:-

1. Maji ya nazi
Maji haya yanauwezo wa kukata kiu vilivyo wakati wa kiangazi au wakati wa joto kali kwani ndani yake yana madini ambayo yataufanya mwili usiendelee kuwa mkavu.

2. Tikitimaji
Hili ni moja ya tunda ambalo linasifika kwa kuwa na maji  mengi lakini pia yenye ladha nzuri, hivyo unashauriwa kutumia tunda hili pale unapohisi joto kuwa kali la mwili.

3. Juisi ya miwa
Ni juisi yenye ladha nzuri na kuongeza nguvu mwilini , lakini pia husifika kwa kuwa na uwezo wa kushusha joto ndani ya mwili.

4. Tango
Hili ni moja ya tunda lililopoa yaani tunda baridi ambalo nalo huweza kushusha joto la mwili pale linapotumiwa na mtu ambaye anahisi joto kali kwa wakati husika.

5. Pamoja na hayo, kunywa maji pia ni miongoni mwa mbinu zenye uwezo wa kushusha joto la mwili.


Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment