Thursday, 13 April 2017

Njia 5 za kufuata kwa wanaume ambao hushindwa kutungisha mimba

Mara kadhaa familia nyingi zinapopata changamoto za kutopata mtoto lawama nyingi huelekezwa kwa mama, lakini kuna wakati kumbe tatizo huweza kuwa kwa baba (mwanaume).

Hivyo leo naomba kueleza haya yafuatayo ambayo yataweza kukusaidia wewe mwanaume au familia ambayo imekaa mda mrefu bila kupata mtoto (watoto) 

Kama mwanaume utaona unashiriki tendo zaidi ya miezi mitatu na kuendelea na mama hashiki ujauzi naomba jaribu kufanya haya yafuatayo:-

1. Hakikisha mwili wako unauzito unaostahili
Yaani usiwe mzito sana kupitiliza kwani hii nayo huweza kuchangia suala la uzazi likawa ni changamoto kwako hivyo zingatia hili nalo kwanza kabla ya kuanza kumlaumu mwanamke.

2. Epuka unywaji wa pombe
Kama unatumia pombe basi jitahidi uache ili kuweza kuwa na nafasi nzuri ya kusababisha mwanamke wako kushika ujauzito kwani unywaji wa pombe pia unaweza kuwa chanzo cha tatizo hili kwa baadhi ya wanaume.

3. Acha kuvuta sigara
Kwa wale wanaume ambao ni mabingwa wa kuvuta sigara nao huweza kuingia kwenye tatizo hili la kushindwa kutungisha mimba kutokana na uvutaji wa sigara hivyo ikiwa unatumia sigara na bado umekuwa ukitafuta mtoto na hupati hebu jaribu kucha kabisa matumizi ya sigara ili upate suluhisho la tatizo hilo.

4. Fanya mazoezi
Kuna baadhi ya kinababa si wafanyaji mazoezi kabisa, hivyo nao huweza kuingia kwenye hatari ya tatizo hili kutokana na kushindwa kutungisha mimba wake zao. Hivyo jitahidi kufanya mazoezi angalau nusu saa kila siku .

5. Epuka msongo wa mawazo.
Hii nayo ni moja ya sababu ambayo huweza kuchangia tatizo hilo la kushindwa kutungisha mimba, hivyo wanaume hushauriwa kuepuka msongo mkubwa wa mawazo linapokuja suala la kutafuta mtoto.

Zingatia
Najua inawezekana hivyo vyote ukavifuata, lakini tatizo likaendelea kama ni hivyo nakushauri ukiona tatizo bado linaendelea jitahidi kufika wewe pamoja na mwenzi wako kwenye kituo chochote cha afya kilicho karibu nawe kwa kupata ushauri zaidi na vipimo zaidi ili kumaliza tatizo hilo.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment