Thursday, 27 April 2017

Unajua kuwa kitunguu swaumu & tangawizi ni msaada kwa wenye pumu?Pumu ni tatizo la kupumua ambalo mara nyingi huwapata watoto na hata watu wazima kutokana na hitilafu mbalimbali katika mfumo wa kupumua.

Pumu huweza kusababishwa na kuvimba kwa kingo za mirija ya kuvuta hewa, matatizo ya mzio (allergy), matatizo ya uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo pamoja na matatizo ya kisaikolojia.

Tatizo hili la pumu likishughulikiwa vizuri kwa watoto wadogo huweza kuisha kabisa.

Mara nyingi tiba ya pumu huwa hailengi katika kuponya kabisa bali husaidai kufifisha nguvu ya mashambulio ya pumu pale yanapotokea, pia kumbukuza kwa kiasi kikubwa idadi ya mashambulio ya pumu kwa mgonjwa.

Moja ya njia inayoweza kutoa ahueni kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja na hii ya kutumia tangawizi na kitunguu swaumu.

Unachopaswa kufanya ni kukatakata na kuponda punje tatu za kitunguu swaumu zilizochanganywa na kiasi kilicholingana na cha tangawizi. Kisha chemsha katika maji glasi moja na unywe kila jioni kabla ya kulala. Fanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni


Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment