Saturday, 15 April 2017

Usikubali upitwe bila kuzifahamu faida hizi za majani ya parachichi

Habari za Jumamosi hii ya kuelekea sikukuu ya Pasaka mdau wetu wa www.dkmandai.com bila shaka umzima wa afya tele.

Leo napenda kuzungumzia kuhusu mmea wa mparachichi hususani yale majani yake ambayo nayo yanauwezo wa kutibu shida mbalimbali ndani ya miili yetu.

Parachichi kama tunda tayari tumeshalizungumza sana, lakini leo napenda tugusie kuhusu majani ya mti wa mparachichi wenyewe.

Matumizi ya majani ya mparachichi yana nafasi kubwa ya kumsaidia mwanamke ambaye hupata maumivu wakati wa hedhi, kinachotakiwa kufanyika ni kupata majani 6 ya mparachichi kisha chemsha kwenye maji lita moja baada ya hapo yaache yapoe kisha tumia maji hayo kwa kunywa glasi moja asubuhi mchana na jioni utaona mafanikio.

Aidha, majani hayo pia husaidia sana kuongeza kiwango cha maziwa kwa kinamama, endapo mama atatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna ni safi na umeliosha vizuri.

Pia majani haya ya mparachichi ni msaada sana katika kutibu majeraha, ili kufanikiwa katika hili unapaswa kusaga majani hayo kisha weka kwenye sehemu yenye jeraha na utaona mafanikio,

Majani ya mparachichi pia husaidia kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na kumuepusha mhusika kukumbwa na vimelea vya magonjwa.

Kwa maelezo zaidi au ushauri wasilina na  Mtaalam Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment