Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 7 April 2017

Vitu 6 vya kuepuka kama unahitaji kupunguza uzito wa mwili

Food to Avoid While on Diet
Watu wengi wamekuwa wakipata shida kuhusu suala la uzito kupita kiasi na kushindwa kutambua namna gani sahihi ya kukabiliana na tatizo hili.

Hapa ninazo njia kadhaa zitakazokusaidia kupunguza uzito wa mwili wako:-

Weka mbali vyakula na vinywaji visivyokuwa vya lazima
Ni vyema kuweka mbali vyakula visivyokuwa vya lazima yaani vile viburudisho kama vile soda na vingine vingi vyenye asili hiyo.

Punguza ulaji wa vyakula vya viwandani
Mara nyingi vyakula vya viwandani si rafiki sana kutokana na maandalizi yake pamoja na matunzo yake vingi huhifadhiwa kwa njia ya chumvi n.k hivyo hufanya kutokuwa rafiki sana kwa wale wenye lengo la kupunguza uzito

Kunywa maji mara kwa mara
Jenga utaratibu wa kunywa maji mara kwa mara hasa kabla ya kula zoezi hili huweza kusaidia kupunguza uzito mkubwa wa mwili endapo zoezi hilo litafanyika mara kwa mara.

Utulivu wakati wa kula

Unapokula hakikisha upo sehemu tulivu na huna shughuli nyingine zaidi ya kula tu, kwani baadhi ya watu hula huku wakiangali runinga au wakichezea simu au kopyuta. hali hii huweza kuchangia mhusika kula zaidi kuliko pale anapokula bila kuwa na shughuli nyingine.

Pata muda wa kutosha wa kulala

Hali ya kukosa usingizi wa kutosha huchangia kuharibu hamu ya chakula, na baadaye kuchangia kuvurugika kwa mpangilio wa mlo wako au ratiba ya kula na hivyo kujikuta ukiingia kwenye tatizo hilo la unene kupita kiasi hivyo ni vyema kupata muda wa kutosha wa kulala kwa faida zaidi.

Punguza matumizi ya vinywaji vyenye sukari
Vinywaji hivyo huchangia kuongezeka kwa tatizo hilo la uzito mkubwa hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vinywaji hivyo ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Epuka matumizi ya pombe pia

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment