Wednesday, 19 April 2017

Yafahamu maajabu matatu kuhusu mafuta haya ya asili

Habari za leo msomaji wangu wa www.dkmandai.com naamini utakuwa mzima wa afya karibu tuendelee kujuzana mambo mbalimbali yakujenga afya zetu zaidi.

Na leo tunaangazia hizi faida 3 za mafuta ya nazi kwetu wanada. Karibu sana

1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo:
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo inauwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya.


2. Mafuta ya nazi huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mafuta ya nazi ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids). hivyo ni mazuri kwa mapishi pia.

3. Hung'arisha ngozi:
Ikiwa unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina hasa ambavyo huathiri ngozi. Pia unaweza  kuyatumia mafuta haya wakati  wa uchuaji wa mwili yaani massage .

Kwa maelezo zaidi au ushauri wasilina na Mtaalam Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment