Thursday, 20 April 2017

Zifahamu kazi 5 za tunda hili lililotajwa kwenye vitabu vya kidini pia

Mtini ni moja kati ya matunda ambayo yametajwa pia katika vitabu vya dini, lakini tunda hili halifahamiki sana miongoni mwa watu wengi licha ya kwamba linafaida nyingi pia ndani ya mwili wa mwanadamu.

Tunda hili limesheheni virutubisho mbalimbali pamoja na madini ambayo huhitajika mwilini

Miongoni mwa madini ambayo hupatakana ndani ya tunda hili ni pamoja na madini ya chuma, 'potassium', zinc, 'copper', 'magnesium' pamoja na 'calcium'.

Kutokana na kuwa na madini ya chuma hulifanya tunda hili kuwa na nafasi nzuri ya kutengeneza seli nyekundu za damu ndani ya mwili na hivyo kupunguza uwezekano wa tatizo la anemia kwa mhusika.

Madini ya magnesium ambayo hupatikana ndani ya tunda la mtini husaidia pia kulinda afya ya nywele, huku madini ya calcium yakisaidi kulinda mwili na kuboresha afya ya mifupa.

Ninazo hapa baadhi ya faida za kiafya za matumizi ya tunda hili la mtini:-
1. Huongeza nguvu ndani ya mwili.
2. Hurekebisha kiwango cha msukumo wa damu ndani ya mwili.
3. Hupunguza hatari ya kukumbwa na kisukari.
4. Hurekebisha umeng'enyaji wa chakula tumboni.
5. Hupunguza kiwango cha cholesterol ndani ya mwili


Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/0784 300 300/ 0769 400 800 au barua dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment