Tuesday, 18 April 2017

Zifahamu sababu 7 za mimba kuharibika mara kwa mara ?
Kuna baadhi ya wanawake kila wanaposhika ujauzito hutoka na kuharibika, lakini wengi hawafahamu chanzo cha tatizo hilo.

Leo naomba nikueleze baadhi ya sababu ambazo huweza kuchangia tatizo hilo kama ifuatavyo:-

1. Magonjwa sugu
Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia.

2. Maambukizi
Kuna magonjwa kama U.T.I magonjwa ya zinaa kama kaswende n.k huwa ni sababu pia ya tatizo hili.

3. Mapungufu kwenye uteru
Mama anapokuwa na matatizo kama uvimbe (fibroid),makovu au vidonda nk huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara.

4. Uzito mkubwa (unene)
Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe.

5. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara
Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika.

6. Utoaji mimba
Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi 9,na kumfanya kila anaposhikapo ikifika miezi kadhaa inatoka tu yenyewe .

7. Matumizi ya Pombe,Sigara
Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo.

Kama unasumbuliwa pia na tatizo hili na hujapata ufumbuzi kwa muda mrefu wasilina na Mtaalam Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com anaweza kukusaidia

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment