Tuesday, 18 April 2017

Zifahamu sababu za mirija ya uzazi kuziba

Tunapozungumzia mirija ya uzazi ya kike. hii ni mirija miwili ambayo kila mmoja huwa huwa upande wake yaani kushoto na kulia na ndio huunganisha kati ya 'ovaries'  (ambapo mayai huzalishwa) na mayai yanapokomaa na kupitia kwenye mirija ya Fallopian kisha yai kukutana na mbegu za kiume na  kuwa fertilized kisha kushuka kwenye uteras (kizazi) tayari kwa uzalishaji.

Hata hivyo mirija hii kunawakati imekuwa ikiathirika kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ndani ya kizazi au maambukizi ukeni ambayo huweza kuchangia mirija hiyo kuziba au kujaa maji na hivyo kuweza kuchangia changamoto wakati wa uzazi kwa mwanamke.

Sasa ni vyema tufahamu sababu za mojakwamoja ambazo huchangia mirija ya uzazi kuziba:-

1. PID (Pelvic Inflammatory Disease) 
Haya huwa ni matokeo ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa mara kwa mara,  ambayo husababisha makovu yenye uvimbe na kusababisha mbegu kutopita. Pia hali hii kunawakati huweza kuchangiwa na upasuaji fulani fulani.

2. Utoaji wa mimba 

Wanawake wenye historia ya kutoa mimba mara kwa mara huweza kuingia kwenye tatizo hili la mirija kuziba kutokana na mirija hiyo kusumbuliwa.

3. Kupasuka kwa appendix  

4. Kufanyiwa upasuaji sehemu ya chini ya tumbo
Hii huweza kuleta madhara endapo upasuaji huo hautafanikiwa vizuri

5. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa

Endelea kuwa karibu na mtandao huu kwani nitahakikisha nakuletea pia na dalili za tatizo la mirija ya uzazi kuziba

Kwa maelezo zaidi au ushauri wasilina na Mtaalam Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment