Tuesday, 25 April 2017

Zifahamu zaidi hizi faida za limao leo


HABARI za leo mdau wetu wa www.dkmandai.com karibu katika muendelezo wetu wa kujuzana mambo mbalimbali kuhusu mimea tiba, matunda pamoja na nafaka leo tuna hii ya limao na maji.

Kwanza kabisa maji yenye mchanganyiko wa limao ni mazuri kwa kusaidia wale wenye shida ya maumivu ya viungo (joints) kwani husaidia sana kupunguza maumivu sehemu mbalimbali za maungio ya mwili pamoja na misuli.

Maji ya moto ambayo yamechanganywa na limao, hutoa msaada wa kurekebisha mfumo wa umeng’enyaji wa chakula mwilini.

Maji ya limao pia husaidia kusafisha ini na kuhamasisha utoaji wa sumu mwilini.

Pia maji haya haya yenye limao husaidia sana wale wenye matatizo katika mfumo wa upumuaji hususani wale wenye vidonda koo au wenye tatizo la mafindofindo (tonsils)

Mchanganyiko wa maji na limao pia husaida sana kusafisha damu mwilini pamoja na mishipa ya damu yenyewe.

Halikadhalika matumizi ya maji yenye limao husaidia sana kuimarisha afya ya ngozi kutokana na kuwa na vitamin C ambayo huboresha ngozi zetu. Hivyo ni vizuri kunywa maji ya limao mara kwa mara asubuhi ili kuboresha hali ya ngozi zetu.

Unywaji wa maji ya limao pia husaidia kuzuia saratani mbalimbali kutokana na limao kuwa na alkaline, tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa saratani huwa ni ngumu kustawi sehemu yenyewe yenye alkaline

Mbali na hayo, pia husaidia kupunguza maumivu ya meno pamoja na kusaidia kupunguza uzito.

Kama utahitaji maelezo zaidi kuhusu mada hii naomba wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment