Friday, 28 April 2017

Zingatia mambo haya 10 ili uishi maisha marefu yenye afya


Kuna baadhi ya mambo yakizingatiwa katika maisha ya binadamu huweza kuwa na faida mbalimbali za kiafya ikiwa ni pamoja na kuishi maisha marefu na yenye afya tele kwa mhusika.

Mambo hayo ni pamoja na haya hapa chini:-

1. Epuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi au kuweka mafuta mengi kwenye vyakula.

2. Epuka kutumia sukari nyingi

3. Jenga utaratibu wa kupima afya yako kila mara au kuwaona wataalam wa afya kila baada ya mda fulani.

4. Acha au punguza kutumia vinywaji kama pombe na juisi/ soda za viwandani .

5. Pata wakati wa kupumzika

6. Hakikisha unaishi sehemu yenye hewa safi

7. Hakikisha unalala kwenye kitanda chenye chandarua wa kuzuia mbu na nyavu madhubutu kwenye madirisha ya nyumba yako.

8. Epuka kushiriki ngono zembe

9. Epuka ulaji wa vyakula vya magengeni na vile vinavyotembezwa barabarani.

10. Zingatia ulaji wa matunda kila siku na kunywa maji ya kutosha

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na nyingine nyingi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.


No comments:

Post a Comment