Friday, 26 May 2017

Aina 3 ya vinywaji na vyakula vyenye nafasi ya kuondoa mawe kwenye figo

pomegranate juice 620
AFYA ya figo ni muhimu kama ilivyo afya ya moyo, hii ni kwa sababu figo ni moja ya kiungo ambacho husaidia kuchuja sumu mbalimbali ndani ya mwili na baadaye kutoa taka mwili kwa njia ya haja ndogo (mkojo)

Matatizo ya figo huweza kuchangia ugumu wa upatikanaji wa haja ndogo (mkojo) au miguu na mikono kuvimba.

Pia mtu mwenye shida ya figo huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo ya moyo.

Leo nimeona nikwambie kuhusu hivi vyakula na vinywaji kadhaa ambavyo huweza kumsaidia mtu mwenye shida ya mawe kwenye figo.

1. Tende
dates
Ni moja ya tunda ambalo hutumika sana katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, lakini pia inaelezwa kusaidia watu wenye shida ya mawe kwenye figo endapo itatumika mara kwa mara.

Jinsi ya kutumia unatakiwa kuloweka usiku kucha tenda hizo kwenye maji safi kisha asubuhi toa mbegu zake halafu tumia maji hayo kumpatia mtu mwenye shida ya mawe kwenye figo.

2. Tikitimaji
watermelon 620x350
Matumizi ya tikiti maji huweza kuwa msaada kwa mtu mwenye shida ya mawe kwenye figo kutokana na kuwa na madini ya potassium, chumvi ndani yake ambayo husaidia kurekebisha kiwango cha acid kwenye haja ndogo (mkojo). Hta hivyo matokeo mazuri ya juisi hii utaweza kuyapata endapo itachanganywa na kiungo fulani ambacho sana sana hutumiwa na wahindi.

3. Juisi ya komamanga
pomegranate juice 620
Mbegu pamoja na juisi ya komamanga ni vitu muhimu sana kwa afya ya figo kutokana na uwezo wake wa kuondoa mawe kwenye figo. Hii ni kutokana na juisi hiyo kuwa ni chanzo kizuri cha madini ya potassium.

Zingatia
Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

Source: Smart Cooky

No comments:

Post a Comment