Wednesday, 10 May 2017

Dalili 4 zinazoashiria kuwa mwili wako umepungukiwa madini ya 'potassium'

blood pressure
Miili yetu huhitaji virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamini na madini mbalimbali ili kuendelea kubaki na afya njema.

Mara zote vitamini hizo pamoja na madini hayo hutokana na vyakula na vinywaji tunavyokula kila siku katika maisha yetu.

Kuna baadhi ya vitamini au madini fulani yanapokosekana mwili huweza kusababisha madhara kadhaa ya kiafya kwa mhusika.

Leo nataka nieleze madhara kadhaa ambayo huweza kujitokeza kwa mtu ambaye anashida ya upungufu wa madini ya potassium mwilini mwake.

1. Kuweza kusababisha shinikizo la damu
Hii ni kwasababu madini ya potassium husaidia mishipa ya damu kurelax hivyo inapokosekana huweza kuchangia mishipa ya damu kushindwa kusinyaa na kutanuka ipasavyo na hivyo kuchangia tatizo la shinikizo la damu.

2. Husababisha kuwa na misuli isiyo imara
Madini ya potassium huenda kufanya kazi ya kuimarisha afya ya misuli ndani ya mwili na hivyo kuifanya kuwa madhubuti zaidi.

3. Kuhisi hali ya kizunguzungu
Kiasi cha kutosha cha madini ya potassium husaidia kuweka sawa mwenendo wa mapigo ya moyo hivyo kumfanya mhusika kutohisi kizunguzungu. Hivyo madini hayo yanapokosekana huweza kumfanya mhusika kuhisi hali hiyo.

4. Kubana kwa misuli 
Unaweza kujikuta ukipatwa na hali ya kubanwa kwa misuli hasa miguuni pale unapokosa madini ya potassium ya kutosha mwilini mwako

Zingatia
Madini ya potassium unaweza kuyapata kwa kujenga utaratibu wa kula ndizi mbivi kila siku kwani tunda hilo lina kiwango kikubwa cha madini hayo ambayo huweza kumsaidia mhusika kuondokana na matatizo hayo yaliyotajwa hapo juu.

bananas
Unaweza kula angalau ndizi mbili kila siku kwa matokeo mazuri zaidi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment