Thursday, 11 May 2017

Fahamu kuhusu faida za soya na namna ya kuiandaa


Maharage ya soya ni moja ya vyanzo vizuri vya virutubisho katika miili yetu. Kutokana na kuwa na kiwango kizuri cha protini kiasi cha asilimia 40%.

Pia soya imejaliwa kuwa na kiwango kidogo cha mafuta ambayo pia hayana lehemu.


Miongoni mwa faida ya mharage ya soya au unaweza kuiita soya lishe ni pamoja na kusawazisha kiwango cha  sukari mwilini hivyo kupambana na ugonjwa wa kisukari.

Pia soya lishe huweza kuwasaidia wagonjwa wa figo pamoja na moyo, huku ikisaidia kukinga dhidi ya matatizo ya saratani hususani ile ya kibofu  pamoja na magonjwa mengine ya wanawake.


Leo napenda pia nikueleze namna ya kuandaa unga wa soya au soya lishe msomaji wangu.

Mahitaji

 • Maharage ya soya kiasi kinachokutosha • Sufuria • Chujio • Maji  • Ungo.


Namna ya kutengeneza

 • Anza kwa kusafisha soya yako kwa kuondoa mawe na yale maharage ya soya yaliyooza au uharibika. kisha yapete ili kuondoa vumbi, lakini usiyaoshe. • Kisha yaweke maharage yako ya soya kwenye maji ya moto ambayo tayari umeshainjika jikoni yachemshe kwa takribani dakika 30 , lakini hakikisha unachemsha maji kwanza ndipo uweke maharage yako ya soya. • Baada ya kuyachemsha, ipua sufuria kisha yaondoe maharage na kuyaweka kwenye sufuria au beseni iliyo na maji yasio ya moto.
 • Kisha ondoa maganda kwa kupekecha maharage yako ya soya kwa mikono halafu mwaga maji hayo taratibu kutoa maganda ambayo umeyapekecha rudia tena kwa kutoa maganda kwa vidole hadi yaishe. • Baada ya hatua hiyo utaanika maharage yako ya soya juani kwa muda ambao utaonayamekauka vizuri. Hakikisha unayaanika sehemu nzuri isiyo na vumbi, wadudu au uchafu wa aina yoyote. • Baada ya maharage kukauka vizuri anua kisha yapete na kuyapeleka mashine ya kusaga au yatwange kwenye kinu safi . Lakini mashine ni nzuri zaidi ili kupata unga wenye ubora na kiasi kizuri pia. • Kisha chukua chujio uliyoiandaa anza kuchuja unga huo vizuri kwa aliyetwanga ni vizuri akarudia kutwanga mabaki ya maharage ili apate kiwango kizuri cha unga.
ZINGATIA

Unaweza kutumia unga utokanao na soya (Soya lishe) kwa kuweka kwenye supu, mchuzi na hata kutengenezea bidhaa kadhaa kama vile mikate.

Kwa maelezo zaidi au ushauri kuhusu lishe na matatizo mengine unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai moja kwa moja kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment