Tuesday, 9 May 2017

Fahamu manufaa ya maji yenye mchanganyiko wa limao

Unywaji wa maji ya moto ni moja ya tiba ambayo mtu binafsi anaweza kuiandaa na kujitibia mwenyewe akiwa nyumbani na ikawa moja ya kinga ya magonjwa mbalimbali kwa mhusika.

Mtaalam Mandai anasema matumizi ya maji ya moto husaidia kuyeyusha mafuta tumboni, kusafisha haja ndogo, kutoa sumu mwilini na kurahisisha mzunguko wa damu.

Mtaalam huyo, anasema maji yanasaidia sana kurahisisha uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini, hivyo kuna haja ya watu kuzingatia kunywa maji ya moto ambayo hufanya kazi haraka bila kuchosha figo.

Aidha, maji ya moto yanapochanganywa na ndimu au limao na kutumiwa kabla ya kifungua kinywa husaidia kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.

Mtaalam huyo anaeleza kuwa maji ya moto ni mazuri zaidi kuliko yale ya baridi, hii ni kwa sababu maji ya moto huanza kufanya kazi moja kwa moja pindi yanapofika mwilini, lakini yanapokuwa ya baridi ni lazima yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.

Pia maji hayo ya moto, humsaidia mtumiaji kuepuka hatari ya kuumwa tumbo, hususani pale anapokunywa maji ya baridi pasipo kutanguliza kitu chochote tumboni. Lakini yanapokuwa maji ni ya moto inakuwa ni sawa kama umekunywa chai ya kwaida tu.

Hata hivyo, Mandai anasema maji yanayopaswa kutumika ni yale ambayo yamechemka vizuri na kisha kuachwa yapoe na kuwa ya uvuguvugu kiasi.

Pia anasema kuwa wataalam wa tafiti mbalimbali wanasema maji ni muhimu sana katika afya ya mwili na yanapokuwa ya moto huwa bora zaidi, kwani huweza kusaidia kumuondolea mhusika tatizo la mkojo wa rangi ya njano na kuufanya kuwa msafi.

Maji ya moto pia ni msaada mkubwa kwa wale wenye lengo la kupunguza uzito wa miili yao na kuifanya kuwa katika hali ya usawa. Vilevile huchangamsha utendaji kazi wa ubongo.

Mbali na hayo,mtaalam huyo anasema maji moto yamekuwa msaada mkubwa katika usafishaji watumbo, uyeyushaji wa chakula na huwasaidia wale wenye shida ya kupata haja kubwa, sambamba na kuongeza kinga mwilini hasa pale asali na limao vitakapoongezwa.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment