Wednesday, 3 May 2017

Fahamu namna binzari inavyoweza kutatua tatizo la maumivu ya miguu

Maumivu ya miguu ni moja ya tatizo ambalo limekuwa likiwakabili watu wengi kwa sasa, miaka ya nyuma tatizo hili lilikuwa likiwakabili zaidi watu wenye umri mkubwa, lakini kwa sasa tatizo hili limekuwa likiwakabili hata baadhi ya vijana.

Tatizo hili huweza kuwa ni la mguu mmoja au hata miguu yote miwili na sababu za matatizo haya huchangiwa na mazingira ya kazi ya mhusika au uchovu wa misuli, ukosefu wa lishe bora, upungufu wa maji mwilini au kusimama kwa muda mrefu n.k

Sasa basi leo naomba nikueleze msomaji wangu kuhusu huu uwezo wa binzari au wengine huiita manjano  kutatua tatizo hili endapo yakitumika vizuri.

Kinachohitajika kufanyika ni kupata kijiko kimoja cha unga wa manjano au binzari pamoja na mafuta ya ufuta kisha changanya kidogo halafu tumia mchanganyiko huo kupaka sehemu yenye maumivu.Huku ukichua kwa taratibu.

Baada ya kupaka mchanganyiko huo kaa nusu saa kisha nawa vizuri kwa maji ya uvuguvugu na ufanye zoezi hilo la kutumia mchanganyiko huo mara mbili kwa siku hadi utakapopata nafuu kabisa.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment