Saturday, 13 May 2017

Fahamu umuhimu wa tikitimaji kwa kinamama wajawazito


TIKITIMAJI ni moja ya matunda yanayolimwa sana katika maeneo mbalimbali nchini hususani maeneo yenye kiwango fulani cha hali ya joto.

Inakadiriwa kuwa asilimia 92 ya tunda hili ni maji, lakini licha ya kuwa na maji hayo yenye ladha nzuri.

Tikitimaji ni chanzo cha virutubisho mbalimbali ndani ya mwili wa mwanadamu ikiwa ni pamoja na vitamin A ambayo husadia kuimarisha afya ya macho.

Leo napenda tufahamishane zaidi kuhusu umuhimu wa tunda hili kwa mamamjamzito.

Hupambana na mfumo mbovu wa umeng’eji chakula tumboni

Mara nyingi mwanamke anapokuwa mjamzito huweza kukumbwa na tatizo la kukosa choo, lakini matumizi ya tunda la tikitimaji hasa juisi yake huweza kuwa suluhisho la tatizo hilo.

Matumizi ya tikitimaji pia husaidia kuzuia tatizo la mwili kuvimba
Wanawake wengi wanapokuwa katika hali ya ujauzito baadhi yao hupatwa na matatizo ya miguu kuvimba au mikono, hivyo matumizi ya tikitimaji huweza kutatua tatizo hilo kutokana na tunda hilo kuwa na madini ambayo huweza kuzuia mishipa ya damu isizibe.

Tikitimaji pia husaidia kupambana na homa za asubuhi ‘Morning sickness’
Inaelezwa kuwa tunda hili ni nzuri kwa wanawake wajawazito kwani husaidia kuzuia kichefuchefu hususani asubuhi, Tikitimaji huwa na nafasi kubwa ya kutuliza hali ya kichefuchefu hivyo kwa wanawake ambao hukumbwa na hali hiyo ni vyema kutumia tunda hili.

Tikitimaji pia husaidia kuzuia upungufu wa maji mwilini

Tunda hili husifika kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maji, hivyo hufaa kwa wanawake hususani wanapokuwa katika hali ya ujauzito.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment