Saturday, 27 May 2017

Faida 4 za kufunga mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan


Kwa mujibu wa dini ya kiislam tunakumbushwa kuwa kila muislam mzima na mwenye afya njema anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya kufunga chakula na kinywaji mcahana na kutwa sambamba na kujizuia kushiriki toka alfajiri hadi magharibi.

Pamoja na hayo, matendo hayo yatoba hupaswa kuendana na kuswali sana pamoja na kusoma quran kwa wingi.

Katika mwezi huu wa Ramadhani kadhalika inatakiwa kwa muislam kuwa mengi ya maneno yake yawe katika kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwani ni jambo ambalo linasaidia katika kuusafisha moyo  wake na kuiboresha funga yake.

Mbali na hayo zipo pia faida nyingine za kufunga kama zifuatazo

1. Ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu alizotuteremshia na faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi siku ya mwisho.

2. Faida ya pili ya mfungaji wa swaumu ni kujizoesha kuwa na subira, yaani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mtu anajifunza jinsi ya kuwa mvumilivu na kustahamili njaa, kiu na matamanio ya kimwili.

3. Faida nyingine ni kuwa muadilifu na kujifundisha usawa baina ya masikini na  tajiri.

4. Pia funga hutusaidia kiafya kwani huifanya mifumo kadhaa ya mwili nayo kupata wasaa wa kupumzika kwa mda fulani.

Baada ya hayo yote Mandai Products Company Limited inapenda kuwatakia mwezi mtukufu wa Ramadhani waumini wote wa dini ya kiislam nchini.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

Kwa ushauri zaidi au maoni tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment