Saturday, 6 May 2017

Faida 5 anazozipata mtu anayekula mboga aina ya choroko

Kuna baadhi ya mboga si rahisi sana kuzipata kwenye maeneo yetu ya nyumbani ya kila siku na hata katika migahawa yetu ya vyakula.

Mfano wa mboga hizo ni pamoja na choroko, hii ni mboga ambayo inataka kufanana na maharage isipokuwa yenyewe huwa ni madogo kwa umbo.

Baadhi ya watu huweza kuzitumia kwa kutengeneza bagia ambazo nazo huwa na ladha nzuri zaidi.

Hata hivyo,  licha ya choroko kutotumiwa na watu wengi lakini inafaida zake ndani ya miili yetu wanadamu.

Hivyo leo naomba tuziangalie hizi  faida za kutumia choroko kiafya.
1.Choroko ni kati ya mboga yenye kiwango kikubwa cha protini.

2. Pia choroko zimesheheni  na madini ya phosphorus, calcium na hivyo kusaidia kuimarisha afya ya mifupa mwilini.

3. Mbali na hayo, choroko pia husaidia kulinda afya moyo 

4. Pia husaidia katika masuala ya umeng’enyaji wa chakula tumboni. 

5. Ndani ya mboga hii pia kuna vitamin B1, B2 ambayo husaidia sana kuimarisha mfumo wa fahamu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment