Saturday, 13 May 2017

Hivi ndivyo juisi ya karoti inavyoweza kuondoa sumu za mwilini


Karoti ni moja ya kiungo ambacho wengi tunakifahamu na huwa tunatumia kwa kuweka kwenye baadhi ya chakula kwa lengo la kuleta ladha pamoja na muonekano mzuri wa chakula.

Karoti imesheni virtubisho vingi na muhimu sana ndani yake pamoja na madini ambavyo vyote kwa pamoja hutusaidia sana kukinga na kutibu dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya uoni hafifu, ngozi, nywele na kucha n.k

Unywaji wa juisi ya karoti kila siku ni mzuri na ni vyema ukafanya hivyo kama unaweza hii ni kutokana na faida za juisi hiyo kiafya, lakini pia pamoja na utamu wa juisi hiyo.

Matumizi ya juisi ya karoti yatakufanya kuwa na kinga za mwili imara pamoja na kukulinda dhidi ya magonjwa ya moyo. Hii ni kutokana na karoti kuwa na vitamin A ya kutosha ambayo husaidia kuimarisha mfumo wa kinga za mwili.

Pia uwezo wa vitamin A ndani ya karoti huchangia sana kuongeza uoni mzuri wa macho pamoja na kukuweka katika nafasi nzuri ya kuepukana na mgonjwa ya moyo na kiharusi ‘stroke’

Juisi ya karoti ina nafasi nzuri ya kuondoa sumu hatari mwilini yaani 'Cholesterol' , hii ni kwa sababu ndani ya juisi hiyo huwa na madini ya potassium ambayo husaidia kupunguza kiwango cha sumu mwilini.

Aidha, juisi ya karoti pia inasifika kwa kuimarisha mifupa, kutokana na madini ya potasium yopatikana ndani yake ambayo husaidia sana kujenga mifupa mwilini.

Kinga dhidi ya saratani, karoti pia hutumika kama kinga ya matatizo ya saratani husani saratani ya kibofu cha mkojo, saratani ya matiti na tumbo.

Juisi hii husaidia sana katika kumlinda mtoto dhidi ya maambukizi hatari hasa pale inapotumika ndani ya miezi mitatu ya awali.

Juisi ya karoti ni chanzo kizuri cha vitamin zote zinazohitajika kwenye ngozi na kuimarisha afya ya kucha pia

Hayo ni machache kuhusu juisi ya karoti endelea kutembelea tovuti hii kila siku ili kuyajua mengi kutoka kwetu, unaweza kutupigia simu kwa namba zifuatazo: 0784 300 300, 0769 400 800, 0716 300 200 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment