Friday, 26 May 2017

Ishara 5 zitakazokuonesha kuwa mwili wako unakiwango kikubwa cha sukari

Picha kwa msaada wa mtandao
Mara kadhaa najua utakuwa umesikia kuhusu madhara ya matumizi ya sukari kupita kiasi kutokana na kuwa na madhara kadhaa ndani ya miili yetu.

Matumizi holela ya sukari huweza kuchangia matatizo kama vile uharibifu wa figo pamoja na kuongeza hatari zaidi ya magonjwa ya moyo.

Leo nimeona tuelezane kuhusu ishara au dalili ambazo huonesha kuwa mwili wako unakiwango kikubwa cha sukari.

1. Kuhisi uchovu sana na usingizi, hii hutokea zaidi mara baada ya kumaliza kula chakula chenye kiwango kikubwa cha sukari. Hivyo unapohisi hali hiyo mara baada ya kula tambua kuwa mwili wako wakati huo umeupatia kiwango cha juu zaidi cha sukari.

2. Mabadiliko ya kupumua
Mara nyingi unapokula chakula chenye kiwango kikubwa zaidi cha sukari huweza kupelekea mabadiliko ya upumuaji na kuongezeka, hivyo uonapo dalili hizo tambua kuwa kiwango cha sukari kimezidi mwilini mwako kwa wakati huo.

3. Shinikizo la damu, matumizi ya kupindukia ya sukari kwa kiasi kikubwa huchangia tatizo la shinikizo la damu

4. Kuongezeka kwa kiwango cha cholesterol (sumu mwilini), ambayo huchangia magonjwa ya moyo ikiwa ni sababu ya matokeo ya viwango vya juu vya cholesterol.

Zingatia
Tunatoa ushauri mbalimbali kuhusu lishe asili na masuala kadha wa kadhaa kuhusu afya yako, hivyo usisite kutupigia simu muda wowote kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au tutumie barua pepe kupitia dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.


No comments:

Post a Comment