Tuesday, 2 May 2017

Kwa wanawake: Njia asili itakayokufanya kuwa na mikono nyororo

Kinadada wengi hasa wale waishio maeneo ya mijini huwa wanapenda mikono yao kuwa laini na yenye muonekano mzuri.

Pamoja na kupenda aina hiyo ya mikono lakini wapo ambao hushindwa kuwa na mikono ya aina hiyo yenye ngozi nyororo.

Sasa hapa naomba nikueleze wewe dada ambaye unahitaji kuwa na ngozi laini ya mikono yako unachopaswa kufanya ni hii njia ifuatayo:-

Unachopaswa kufanya ni kuchemsha viazi mviringo kisha viponde ili kupata rojo yake na baadaye tumia rojo hilo kupaka mikononi mwako kwa kusugua taratibu na kisha kaa nayo kwa muda wa dakika10 ili kupata matokeo mazuri zaidi.

 Fanya zoezi hili mara kwa mara ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment