Wednesday, 24 May 2017

Mambo 5 muhimu yakuyafanya mwanamke anapojigundua ni mjamzito

Baadhi ya wanawake waapojigundua kuwa ni wajawazito wamekuwa ni wazito kufika kwenye vituo vya afya na kukuta na wataalam ili kupatiwa utaratibu sahihi wa kuishi na hali hiyo. Jambo ambalo kuna wakati limekuwa likichangia mimba kuharibika au vifo visivyokuwa vya lazima.


Hapa leo napenda tufahamishane haya mambo ya msingi ya kuyafanya mara tu unapojigundua kuwa ni mjamzito:

Kupima wingi wa damu;
Upungufu wa damu wakati wa kipindi cha ujauzito ni moja ya sababu inayoweza kuchangia kifo kwa mama na mtoto.

Kupima virusi vya Ukimwi.

Kipindi hiki ni muhimu sana kujua afya yako ikiwa ni pamoja na kupima virusi vya ukimwi na endapo itafahamika wewe ni muathirika utapata faida kuu mbili; kwanza kupewa dawa za kuzuia maambukizi ya mtoto aliyeko tumboni na wewe pia kuishi vizuri na kuwasaidia kuwalinda wale uwapendao.

Kipimo cha choo ndogo na kubwa

Hii husaidia kugundua kama hakuna ugonjwa wowote wa njia ya mkojo kwani ugonjwa wa uti huweza kuleta uchungu na kutoa mimba lakini pia huwasumbua sana akina mama kipindi cha ujauzito.

Kuhusu choo kubwa hii nayo hupimwa kwa lengo la kuangalia minyoo kwani baadhi ya minyoo hutumia damu kama chakula na inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini kwa mama mjamzito.

Kupima malaria
Huu ni moja ya magonjwa ambayo huchangia sana vifo vya kinamama wajawazito na watoto ndio maana serikali ya Tanzania imekuwa ikihamasisha sana mama wajawazito wanatumia vyandarua siku zote wakati wa kulala, lakini wakati huo huo serikali imekuwa ikitoa vidonge vya SP katika kipindi fulani cha ujauzito ili kujuia malaria. Madhara ya ugonjwa huu huweza kuchangia mimba kutoka.

Kupima magonjwa ya zinaa

Haya ni yale magonjwa ambayo huenezwa kwa njia ya ngono, hivyo ni vizuri kupima kaswende na magonjwa mengine ya zinaa kama gonorea nk, ambayo huweza kuleta madhara kwa mtoto tumboni ikiwa ni pamoja na upofu kwa mtoto na hata kifo pia wakati mwingine.

Pia ni vyema kuhudhuria kliniki mara tu unapogundua kuwa unaujauzito ili kuanza kupata maendeleo ya mwanao tumboni.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment