Friday, 19 May 2017

Mambo 5 ya kuzingatia wakati wa kumlisha mtoto

Picha kwa msaada wa mtandao

Habari za leo mpendwa msomaji wa www.dkmandai.com, karibu sana katika muendelezo wetu wa kuhakikisha unapata elimu ya afya kila siku ikiwemo masuala ya lishe asili bora

Leo nimeona tuwakumbuke watoto ili kuwahakikishia usalama wao katika mazingira ya kula.

Ukweli ni kwamba familia nyingi kwa sasa zimekuwa zikiishi na kinadada wa kazi (house girl) ambao ndio kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakishiriki katika kuwatunza watoto nyumbani na kuhakikisha wanakula vizuri na kushinda katika hali ya usalama.

Hivyo ninayofuraha kukumbusha wewe mzazi pamoja na dada wa nyumbani au mlezi mambo haya machache ya kuzingatia katika kuhakikisha usalama wa mtoto wakati wa kula;

1. Jambo la kwanza hakikisha haumuachi mtoto mdogo na chakula au kinywaji bila uangalizi hata kama ni maziwa ya chupa, kama utasahau na kumuacha mtoto katika hali hiyo huweza kusababisha mtoto akapaliwa.

2. Pia usimpe mtoto chakula au maziwa akiwa amelala, analia au anacheka huweza kusababisha mtoto kupaliwa.


3. Epuka kumpa chakula ambacho kinaweza kumkaba au kumpalia hususani karanga, mahindi, zabibu n.k


4. Kabla ya kumpa mtoto chakula hakikisha umekiangalia joto lake usije ukamuunguza mdomo.


5. Mbali na hayo yote, pia usafi wa mtayarishaji, mlishaji na mlishwaji (mtoto) ni muhimu sana katika afya ya mtoto.

Unaweza kuwasiliana nasi pia kama unahitaji kujua masuala mbalimbali kuhusu lishe bora kwa maelezo zaidi tupigie kwa simu namba  0716 300 200/ 0784 300 300/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment