Tuesday, 2 May 2017

Mambo 5 yatakayokuepusha kupata kijinyama kwenye haja kubwa (bawasiri)

Karibu tena msomaji wangu leo tuangazie kuhusu tatizo la bawasiri au kuota kijinyama sehemu ya haja kubwa.

Sasa leo naomba tuelezane  kuhusu hizi mbinu 5 ambazo huweza kusaidia kuepuka kupatwa na tatizo hili.

1. Kwanza ni kuzingatia ulaji wa lishe bora ikiwa ni pamoja na matumizi ya mboga za majani, matunda pamoja na kutumia nafaka zisizokobolewa halikadhalika na vyakula vyenye nyuzinyuzi za kutosha.

2. Kujitahidi kunywa maji ya kutosha angalau glasi 6 kwa siku nzima

3. Epuka kukaa na haja kubwa kwa muda mrefu, jitahidi pale unapohisi haja kubwa nenda kamalize haja hiyo haraka iwezekanavyo.

4. Epuka kukaa muda mrefu sehemu moja, unaweza kukaa baada ya muda kisha ukainuka na kutembea tembea kidogo kisha ukakaa tena.

5. Jitahidi kufanya mazoezi ya viungo nayo huwa na nafasi nzuri ya kukuepusha na tatizo hili.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment